Unalikumbuka lile chama la Napoli pale kwa watu wa soka nchini Italia? SSC napoli ilikuwa hatari chini ya mfanyakazi wa benki ambaye pia ni mzaliwa wa Napoli, Sarri.
Soka la Sarry lilitambulika kama Sarrismo ila nchi ya Malkia Elizabeth namaanisha visiwa vya England wanaliita Sarriball, huyu bwana kwenye mpira burudani ni balaa soka lake lina tuvitu vitu yani ni kama kumuangalia Mbrazil Neymar akipiga Kontrol.
Sarri lile soka lake lilitaka vitu viwili, ‘possession and progression’ unamiliki mpira na kutembea kwenda mbele, Sarri hakuamini sana kwenye issue za kukaa na gozi la mnyama nyuma badala yake alikua akipata mpira anasongesha timu mbele. Timu yake ilicheza sana 4-3-3, kwenye kujilinda ni 4-5-1, Sarri alimwamini kila mchezaji wake kuwa ni ball player, hakutaka maguvu mengi kama Phil Jones.
Anaekumbuka zile pasi za pembe tatu (triangular passing) za Napoli anyooshe kidole juu, anaemkumbuka Jorginho kama mboni ya falsafa hii afanye kama anajikuna, Jinho na Allan wale watoto wa Kibrazil waliswitch sana, Bila mpira walikuwa wanakabia juu( high line play) wakiforce mpinzani apige pasi za kurudi nyuma au kufanya makosa.
Falsafa ya Sarri ilitubadilishia winger Dries Mertens kwenda straika baada ya kuondoka kwa Milki na Higuain, huyu Mertens kila mechi alikuwa kambani, hawa Napoli bwana, wataendelea kumkumbuka Sarri kama mkongwe wao, Wao wanamuita (master of footbal)
Povel
Kocha Bora pale