McQueen kwa Mkopo Middlesbrough

Kijana machachari kutoka Southampton, Sam McQueen rasmi sasa anajiunga na Middlesbrough. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 ni zao kutoka katika mfumo wa vijana wa Southampton, anauwezo wa kucheza mbele na nyuma upande wa kushoto.

McQueen anajiunga kwa Middlesbrough kwa msimu mzima kwa mkopo, ameichezea Southampton mara 50 mara 20 kati ya hizo ni ligi ya Premier. Mchezo wake mkubwa wa kwanza ulikuwa katika ligi ya EUROPA miaka miwili iliyopita. anakuwa kijana wa sita kusajiliwa kwa mkataba wa kudumu, anaungana na Aden Flint, Paddy McNair, Andy Lonergan , Jordan Hugill na  Mo Besic McQueen anatarajiwa kuvaa jezi namba 14 msimu huu.

3 Komentara

    Gud news

    Jibu

    Habar nzuri

    Jibu

    Asanteh kwa taarifa meridianbet!!

    Jibu

Acha ujumbe