Misri Kuandaa Fainali za AFCON!

Hapo awali Cameroon walipewa nafasi ya kuandaa fainali za michuano hiyo mikubwa na ya aina yake Afrika, lakini kutokana na sababu mbalimbali wameweza kupokwa nafasi hiyo; huku Misri akipewa ripoti ya kuandaa mashindano hayo kwa sasa. Hadi mwishoni mwa mwaka jana, ilifahamika wazi kwamba mechi zote zitafanyika nchini humo kwa mabingwa hao wa mashindano hayo yaliyopita.

Baadhi ya sababu zilizofanya Cameroon wapokwe nafasi hiyo ya kuandaa michuano mwaka huu, ni kuonekana kukawia kwa uandaaji wa miundo mbinu rafiki itakayowezesha fainali hizo kufanyika. Ambapo uandaaji wa viwanja na maeneo ya kufikia ugeni huo kwa ajili ya michezo hiyo kutokuwa rafiki na ikiangaliwa muda wa michiano hiyo umekaribia sana. Hivyo, hakukuwa na namna kuweza kuangalia taifa ambalo miundombinu yake ni rafiki wakati wote na haiwezi kuchukua muda kuiboresha.

Sababu nyingine ni ya kisiasa zaidi, ambayo inatokana na uwepo wa makundi ya kigaidi karibu na mipaka ya nchi hiyo kitu ambacho kwa kiasi kikubwa kinahatarisha na kingehatarisha usalama wa washiriki. Ifahamike utimamu wa akili kwa wachezaji ni kitu cha muhimu hasa katika ushiriki wa michiano hiyo mikubwa. Uwepo wa Boko haramu katika baadhi ya maeneo ya mipaka ya bchi hiyo imechangia kwa kiasi fulani kuhamisha taifa litakaloandaa kwa mwaka huu.

Wengi waanaweza kujiuliza, kwa nini Misri wamepewa upendeleo huo kuandaa michuano hiyo itakayoanza 15, Juni –13, Julai ikihusisha timu hizo 24 na sio mataifa mengine?

Misri wamepewa upendeleo huo baada ya kurejea waombaji wa kuandaa michuano hiyo mwaka jana, kwa sababu katika takwimu zao kunakuwa na mataifa wanachama ambao huomba nafasi hiyo. Na shirikisho huangalia kwa kina na kujadili kuona ni yupi angefaa kupata nafasi bila upendeleo. Cameroon alipata nafasi hiyo kwa mara ya kwanza lakini nyuma yake kulikuwa na mbadala kama ilivyo kawaida huweka mbadala [emergency] ili kama kuna kikwazo kitatokea mbeleni waweze kujilinda nacho.

Baadhi ya mataifa yaliyokuwa kwenye kinyanganyiro hicho ni Afrika kusini na Misri; na ndipo wao wakapigiwa chapuo ya kuandaa kwa mwaka huu.

Kila kundi linaloshiriki katika michuano hiyo hutoa washindi wawili ambao ni aliyeongoza kundi hilo na aliyefuatia kwa alama katika kundi husika ili kuunda idadi ya washiriki 24. Mpaka sasa kuna mataifa yamekwishajidhihirishia nafasi ya kusonga mbele kutokana na kuwa na alama nyingi kwenye makundi yao. Timu zilizokata tiketi tayari zipo 14 ambazo ni Madagascar, Senegal, Morocco, Mali, Algeria, Nigeria, Kenya, Ghana, Guinea, Ivory coast, Mauritania, Tunisia, Uganda na waandaaji Misri. Wanasubiriwa washindi wengine kumi waweze kufuzu ili kukamilisha idadi hiyo

 

3 Komentara

    Poa

    Jibu

    Safi.

    Jibu

    Gud news

    Jibu

Acha ujumbe