Kutokana na utafiti uliofanywa hivi karibuni, zimetoka takwimu mpya za wachezaji wanaolamba hela nyingi kwenye klabu wanazochezea. Hii inatokana na mishahara yao wanayolipwa na gharama zao za kuuziana kuwa juu kuliko kawaida. Katika takwimu hizo kuna wachezaji wametoka na wengine wameingia; walioshika nafasi hizo za kukusanya mishahara mirefu.
Ronaldo pamoja na kuwa ni mchezaji ghali kwenye ligi ya Serie A, hajafanikiwa kuingia katika takwimu hizo za kumi bora, zilizotoka hivi karibuni. Ifahamike kwamba kwa sasa ndiye anayeshikilia rekodi ya kuchukua mshahara mkubwa ndani ya ligi hiyo: akimzidi mchezaji mwenzake Paulo Dyabala. Hawa wote hawajafanikiwa kuingia katika taarifa hizo kutokana na kuzidiwa na wachezaji wengine; kwa maana hiyo hakuna mchezaji anayewakilisha kutoka ligi za Italia na Ujerumani.
Neymar anayekusanya kiasi cha £206.5m, anaendelea kushikilia rekodi hiyo ya kulipwa pesa nyingi kwa wachezaji wote duniani wanaocheza katika ligi tano kubwa za Ulaya. Aliweza kusajiliwa na PSG akitoka Barcelona kwa usajili ulioishangaza dunia na uliokuwa sio wa kutegemewa kama angeihama klabu hiyo kwa wakati ule. Lengo lake la kuhama ilikuwa ni kukwepa kivuli cha Messi; kwamba hawezi kuonekana mchezaji mwenye thamani kama ataendelea kucheza naye.
Mbappe naye aliweza kusajiliwa kwenye mazingira yaliyokuwa hayaaminiwi kama angeweza kutua PSG kwa haraka kiasi kile, kwa uhamisho uliowafanya matajiri hawa wavunje vibubu vyao kuweza kumnasa mchezaji huyo aliyekuwa anaviziwa na klabu nyingi kubwa barani Ulaya. Anakusanya kiasi cha £193.8m kama sehemu ya malipo yake kwa kile anachokifanya ndani ya klabu hiyo. Kwa aina hiyo ya wachezaji ni dhahiri kwamba PSG inatumia pesa nyingi sana kwa ajili ya kulipa wachezaji wake.
Mchezaji aliyekulia ndani ya viunga vya Barcelona, Lionel Messi anashika nafasi ya tatu katika kukusanya mshahara mkubwa akiwa analipwa na klabu hiyo kiasi cha £183.2m, kiasi ambacho ni kikubwa ukizingatia mchezaji huyu amelelewa na klabu hiyo tangu walipoona kwamba nakipaji hadi sasa ndiye wanayemtegemea kwa kiwango kikubwa katika timu hiuo baada ya wakongwe aliocheza nao kustaafu soka la ushindani.
Wachezaji wengine wanaotengeneza idadi hiyo ni mchezaji wa Liverpool, Mohamed Salah mwenye thamani ya £151.6m akiwa katika nafasi ya nne, Harry Kane wa Tottenham anayekusanya kiasi cha £136.1m, namba sita inashikiliwa na Eden Hazard anayekipiga na Chelsea akikusanya £133.5m, Kevin De Bruyne ambaye ni mhimili wa Man City akiwa anajizolea £116.6m, Antoine Griezmann anayesumbua katika klabu ya Atletico Madrid anaondoka na kiasi cha £113.2m, Paul Pogba wa Man United akisajiliwa kutoka Juventus anakusanya kiasi cha £107.5m na anayefunga hesabu hiyo ya wachezaji wanaoshika pesa ndefu ni Philippe Coutinho aliyejiunga na Barcelona akitokea Liverpool na anakusanya kiasi cha £106.5m.
isha
Hongera sana kwao