Moise Kean Aandika Rekodi Mpya Serie A

Kinda wa Juventus Moise Kean ameandika rekodi mpya kwenye Ligi ya Italia -Serie A baada ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kufunga magoli kwenye mechi 4 mfululizo za Serie A, ameifuta rekodi iliyoandikwa na Mio Balotelli.

Staa huyu mara nyingi amekuwa akifananishwa na Mario Balotelli ambaye alifunga magoli kwenye mechi 3 mfululizo mwaka 2009.

Moise Kean Aandika Rekodi Mpya Serie A

Mkwaju uliotandikwa na Joao Cancelo ulionekana kulilenga goli, lakini golikipa alikuwa mbioni kuunasa huku kijana Moise Kean akimvuruga kipa kwa kumkwepeshea mpira huo.

Kama Juve wakishinda gemu dhidi ya SPAL watakuwa wamejiandikia ubingwa mwingine wa Serie A kwa miaka 8 mfululizo. Kean anakuwa muhimu mno wakati kama huu wakati mastaa kama Cristiano Ronaldo akikosa gemu 2 kwa sababu ya jeraha.

Kinda huyu wa miaka 19 pia amefanya makubwa katika timu ya Taifa ya Italia mwaka huu akifanikiwa kucheka na nyavu kwenye gemu ya kufuzu Euro 2020 wakati wa likizo ya kimataifa.

3 Komentara

    Kean noma sana.

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

    Moise kean ni noma

    Jibu

Acha ujumbe