Msala ni kwa Kocha wa Madrid Kuliko Mourinho!

Wengi wa mashabiki wa kandanda wanamtazama kocha Jose Mourinho wa klabu ya soka ya Manchester United kuwa atafukuzwa klabuni pale ila kiukweli ni kocha wa Real Madrid, Julen Lopetegui ambaye anaonekana kukumbwa na hofu kuu!

Kocha huyu anaweza kupoteza kazi yake ikiwa ni muda wa miezi 3 pekee umepita tangu aanze kazi hiyo. Mpaka sasa tayari amepoteza mechi ya ligi, Ligi ya Mabingwa na Kombe la Super Cup!

Kipindi kocha huyo anatua klabuni hapo mwanzoni kabisa mwa michuano ya kuwania Kombe la Dunia alionekana kupata wakati mgumu sana ikiwa ni mara baada ya kocha Zinedine Zidane kusepa klabuni hapo.

Pamoja na kwamba kocha huyo aliondoka ila kocha huyo ambaye ni raia wa Hispania alijiunga na Real Madrid baada ya staa wake Cristiano Ronaldo kuondoka na kujiunga na Juventus inayokipiga Ligi Kuu ya Italia, Serie A na kumfanya kocha huyo azidi kuwa na wakati mgumu!

Kwa sasa analazimika kutengeneza kila kitu upya ila sasa ubaya wa Real Madrid ni kutochelewesha kocha anayehangaika ambapo hili linamfanya awe kocha mwenye hofu zaidi na kazi yake kwa wakati huu.

2 Komentara

    Duh

    Jibu

    Asanten kwa taarifa meridian

    Jibu

Acha ujumbe