Raisi wa shirikisho la soka Afrika CAF na mmiliki wa klabu ya Mamelodi Sundowns Patrice Motsepe amesema yuko tayari kumlipa mshahara kocha Pitso Mosimane ikiwa ataifundisha timu ya taifa ya Afrika Kusini.
Pitso Mosimane hivi karibuni ameacha kazi kwenye klabu ya Al Ahly, baada ya kudumu kwa muda wa miaka miwili na kufanikiwa kushinda makombe mawili ya klabu bingwa barani Afrika, ligi kuu ya Misri na kombe la Super Cup Afrika, huku akiacha historia ya kucheza fainali tatu za ligi ya mabinga Afrika.
Akiwa kwenye kongamano la SAEditorsForum nchini Afrika Kusini alielezea hisia zakw kwa kocha anayempenda na kunukuliwa, “bila shaka kocha ninayempenda ni Pitso, nampenda sana pitso na nitampenda daima, anasehemu maalum kwenye moyo wangu.
“Namtakia mema, natamani aifundishe timu ya taifa ya Bafana Bafana, nitaitumia Motsepe Foundation kugharamia mshahara wake.”
Alipouliza agharamikie mshahara wake kwani anagharama kubwa, alijibu. “Nadhani ni ubora wake na ubora hauji kirahisi.“
Patrice Motsepe ameshawai kufanya kazi na Pitso akiwa kwenye klabu ya Mamelodi Sundowns kuanzia mwaka 2012 hadi mwaka 2022, huku akifanikiwa kushinda vikombe 11 kwa ujumla.
ALIYA’S WISHES
Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.