KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ leo kimeingia kambini na kuanza mazoezi rasmi ya kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za CHAN dhidi ya Uganda.

Mchezo wa kwanza kwa ajili ya kufuzu CHAN unatarajia kupigwa Agosti 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar huku ule wa marudiano ukitarajiwa kupigwa Septemba 3, mwaka huu kwenye Uwanja wa St. Marys, Uganda.

Stars, Stars Waanza Tizi Kibabe, Meridianbet

Jumla ya wachezaji 25 walioitwa kwenye kikosi hicho tayari wameingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo chini ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Kim Poulsen.

Ikumbukwe Taifa Stars walifika hatua hii baada ya kuwatoa Somalia kwa jumla ya mabao 3-1 ambapo michezo yote ilipigwa kwenye dimba la Mkapa, Dar.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa