Mchezaji mkongwe wa Tanzania Prisons na nahodha wa timu hiyo Benjamini Asukile alifunguka kuwa aliwaambia viongozi na mabosi wake kuwa kwa vyovyote itakavyokuwa lazima wataibakiza timu yao kwenye ligi hiyo.

Asukile aliyasema hayo mara baada ya juzi Jumatano kufanikiwa kuibakiza Prisons kwenye ligi baada ya kufanikiwa kushinda mbele ya maafande wa JKT Tanzania kwenye mchezo wa Play Off kwa jumla ya mabao 2-1 kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya.

Asukile, Asukile: Niliapa Kuibakisha Prisons Ligi Kuu, Meridianbet

Asukile alisema: “Nilikuwa nimehapia mbele ya viongozi wangu na wakubwa wangu kuwa kwa namna ambavyo itakuwa lazima Prisons itabaki ligi haitashuka, kwa sababu ingekuwa jambo baya sana kwetu kuona timu inashuka kwenye miguu yetu.

“Wakati nipo benchi na tayari tulikuwa tumefungwa bao moja, nilikuwa natafakari nitafanyaje ili kuinusuru timu na kutimiza ahadi niliyotoa. Nashukuru Mungu baada ya kuingia nikafanikiwa kufunga na kuibakisha timu ligi kuu.”

Kwa kitendo cha Prisons kubaki ligi kuu kunafanya timu zilizoshuka kuwa mbili na kupanda mbili kutoka Championship na timu zilizocheza Play Off kutoka ligi kuu zikibakia.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa