Klabu ya Geita Gold FC inayoshiriki ligi kuu ya NBC Premier League imekumbana na rungu la shirikisho soka duniani FIFA kwa kuzuiwa kufanya usajiri mpaka pale watakapomlipa stahiki zake aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Ettiene Ndayiragije.

Ettiene Ndayiragije aliipeleka klabu ya Geita Gold FIFA, baada ya klabu hiyo kuvunja mkataba nae na kushindwa kumlipa stahiki zake zikiwemo pesa za kuvunja mkataba na stahiki zingine ambazo alipaswa kulipa, lakini hakulipwa wakati akiifundisha klabi hiyo.

FIFA, FIFA Yatembeza Rungu kwa Geita Gold FC, Meridianbet

FIFA imeamuru klabu ya Geita Gold FC kutokufanya usajiri wowote mpaka pale watakapo mlipa stahiki zake kocha Ettiene Ndayiragije, ikiwa watakaidi na kufanya usajiri basi shauri hilo litapelekwa kwenye kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka duniani kwa ajiri ya maamuzi zaidi.

Hivi karibuni klabu ya Biashara United nayo ilikumbana na shauri kama ambalo Geita Gold wanakumbana nalo sasa, baada ya kushindwa kumlipa mchezaji wake na kupewa adhabu sawa na Geita Gold na waliipuuzia na kupelekea shauri hilo kwenda kamati ya nidhamu na kugongwa nyundo ya miaka miwili pasipo kufanya usajiri.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa