Timu ya Kagera Sugar imeweka wazi kuwa kuelekea kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Simba kuwa watatumia zaidi eneo la kiungo kwa ajiri wa wakabiri wana msimbazi kwa ajiri ya kuibuka na ushindi.

Mchezo huo wa ligi kuu Bara wa mzunguko wa pili unatarajia kupigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Simba, Kagera Kuwawashia Moto Simba, Meridianbet

Akizungumzia maandalizi yao, baraza amesema: “Kwanza tunamshukuru Mungu kikosi kinaendelea vizuri, wachezaji wote wako vizuri na tunaenda kucheza na Simba ni timu kubwa tunawaheshimu ila yote kwa yote tunaenda kutafuta pointi tatu.

“Mipango katika mchezo wa kwanza dhidi ya Azam ilishindikana lakini nawapongeza vijana wangu walijitahidi sana kucheza ila matokeo hayakuwa upande wetu lakini katika mchezo huu tunakuja na mipango mingine.

“Nafahamu kocha wa Simba atakuja na mbinu ya kucheza kwenye eneo la kiungo lakini hata sisi tunajiandaa na tutaenda kufunguka kwahiyo atakaeshika eneo la kiungo ndio ataibuka na ushindi.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa