Wachezaji nyota wa klabu ya yanga Mayele na Aucho ambao walikuwa mapumzikoni wamerejea rasmi kwenye kikosi cha timu hiyo ambacho kimeweka kambi kigamboni Avic Town kwa ajiri ya maandalizi ya michezo ya msimu unaotarajia kuanza hivi karibuni

Yanga ilianza kambi yao kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao chini ya Kocha Mkuu, Nassredine Nabi.

Mayele na Aucho
Mayele na Aucho

Akizungumzia kambi yao, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa mpaka kufikia kesho jumatano wachezaji wote watakuwa kambini kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao.

“Waliokuwepo wachezaji watano ambao hawakuwasili kambini lakini tayari watatu wameshawasili ambao ni Khalid Aucho, Fiston Mayele na Djuma Shaban.


“Kwa upande wa Yannick Bangala na Benard Morrison wao wanatarajia kuwasili leo usiku kwahiyo baada ya kufika tunatarajia na wao kesho wataungana na wenzao mazoezini kuendelea na maandalizi ya msimu mpya.

“Vijana asubuhi hii wameendelea na mazoezi na wakimaliza watapumzika mchana na jioni wataendelea tena na kama mnavyojua sahivi ni dozi tu mpaka kieleweke.”


 


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa