Kocha Joslin amejiunga na kikosi hicho hivi karibuni akichukua mikoba ya Malale Hamsin ambaye mkataba wake ulivunjwa.
Akizungumzia hali ya kambi yao, Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Hassan Juma amesema kuwa “Tunamshukuru Mungu timu inaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao wa ligi.
“Wachezaji wote wapo fiti na kwa sasa bado kocha anaangalia ni jinsi gani ambavyo anaweza kuwajenga wachezaji kisaikolojia ili waweze kupambania timu yao.”