Ikiwa bado takribani wiki mbili ili michezo ya klabu bingwa ya dunia iweze kuanza kutimua vumbi; kila klabu inafanya maandalizi ya awali kabisa kuona kama kuna namna wanaweza kupata ushindi katika mechi hizo. Hiyo ni hatua muhimu sana kwa kila klabu maana kufanya hivyo kunawapa nafasi ya kutambua mapungufu waliyo nayo na kujaribu kuyafukia kwa namna moja au nyingine.

Kuelekea mechi itakayokuwa ya aina yake kati ya Manchester United watakaokuwa wenyeji wa Paris Saint Germain, mchezaji machachari wa klabu hiyo amewatahadharisha mashetani hao kuwa wanahitaji maandalizi makubwa katika mechi hiyo maana kwa namna walivyo na kikosi imara wanategemea kuchukua alama zote mikononi mwao.

Manchester watawakaribisha miamba hao wa soka kutoka Ufaransa na mechi hiyo inategemewa kuchezwa tarehe 14/Februari kwa mzunguko wa kwanza na watarudiana tarehe 6/Machi. Kupitia hilo Neymar anawaambia mashetani wajipange maana wapo vizuri na wanaendelea kujifua wawe vizuri zaidi pia wamejipanga na hawapo tayari kuwapa hata upenyo ili washinde mechi zao zote.

Sio kwamba klabu hiyo ya Ufaransa imejiandaa kupata ushindi katika mzunguko huo tu, wanamalengo ya muda mrefu kuweza kuendea kufanya vizuri hadi hatua ya fainali. Na kiuhalisia kwa sasa; wanachoangalia ni kuandaa mbinu zitakazoweza kuwacharanga wapinzani wao ma kuwafanya wao mabingwa.

Neymar anaonelea kwamba kwa msimu huu wana kila lillilojema kuweza kuleta ushindani na kunyanyua ndoo hiyo. Kuna kipindi aliwahi kuzungumziwa kwamba ni aina ya wachezaji ambao wanaonekana wanaoonekana bado hajakua kisoka kwamba hata anayoyafanya bado yana wasiwasi kubwa na utoto mwingi tofauti na wengi walivyomchukulia apofika ndani ya klabu hiyo.

Pamoja na onyo hilo, Neymar anatambua nafasi ya klabu hiyo kwamba, pamoja na magumu wanayopitia kwa sasa wanaonekana kurejea katika hali yao ya kupambana hivyo inawezekana ikawa mechi ya aina yake kwa namna timu zote zilivyo na wachezaji wenye kasi na wenye uwezo mkubwa kisoka duniani.

Kwake mchezaji mwenzake, Mbappe anaona kwamba kuna ugumu sana juu ya mechi hiyo. Kutokana na wachezaji wa kila timu na  aina ya mifumo yao; lakini wanachokiona juu yao ni kwamba; wachezaji wengi ndani ya kikosi chao hawajakua kisoka kutokana na namna wanavyopambana kuipa timu hiyo imesheheni vipaji vya kila aina ambavyo ilibidi wakati wowote wapate ushindi. Kwake yeye anaona wanahitaji maandalizi mazito sana ya namna wanatakiwa wacheze kwa nidhamu ndani ya michezo husika.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa