Nicolo Barella Anaviziwa na Arsenal

Arsenal wanaripotiwa kuwa wametuma wawakilishi kwa ajili ya kumtupia kijicho staa wa Cagriali Nicolo Barella wakati akijichapia goli lake la kwanza kwenye gemu ya kimataifa akiwana timu yake ya taifa ya Italia.

Nyota huyu mwenye miaka 22 alikuwa akitupiwa jicho kwenye gemu ya ufunguzi wa michuano ya kufuzu EURO 2020 ambayo Italia walipata ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Finland Jumamosi.

Kwa mujibu wa chanzo cha La Gazzetta dello Sport, Arsenal walikuwa wametuma skauti wao kwenye viunga vya Dacia Arena kule Udine kwa ajili tu ya kumtazama vyema kiungo huyu -Barella ambaye alikuwa “Man of the Match!”

Kiungo huyu alifanya vyema kwenye gemu hii huku dau lake likitajwa kuongezeka kufikia kati ya paundi milioni 45-50. Raisi wa Cagliari bwana Tommaso Giulini anasema kuwa huenda dau likazidi zaidi ya hapo.

Klabu zingine zinazohusishwa na mbio za nyota huyu ni pamoja na Napoli, Chelsea na Inter Milan. lakini hakuwa kwenye mpango wa kusepa kwenye dirisha la mwezi Januari.

4 Komentara

    Nicolo Barella n mchezaji mzuri anaechipukia maana sio arsenal tu Kuna club nying ambazo zinamuitaiji Kama Chelsea nk

    Jibu

    Wachezaji km hao wa kufunga magoli ndio wazuri.

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

    Hii safi

    Jibu

Acha ujumbe