Kumekuwa na habari kuwa moja ya timu za kule Uturuki, Fenerbahce inamtamani sana nyota wa klabu ya soka ya AC Milan, M’Baye Babacar Niang na kuwa wameshatangaza kusudi la wao kujitosa kwenye vita ya kuwania kumsajili.
Jarida la L’Equipe limeripoti kuwa vinara hao wa kabumbu nchini Uturuki wanao uhitaji mkubwa sana wa huduma ya nyota huyo ambaye ana umri wa miaka 22.
Inasemekana kuwa kwa sasa wamekwishaandaa ofa ya euro milioni 7 ambazo zinatosha kabisa kufikia paundi milioni 16 ambazo zinatakiwa na AC Milan ili wampate. Tusubiri kusikia zaidi.
Povel
Gud news