Ozil Hana Bahati

Kiungo wa Arsenal aliyejistaafisha kuchezea timu yake ya taifa ya Ujerumani baada ya ripoti mbalimbali, kwa sasa anaonekana kukosa nafaei ndani ya kocha mpya wa klabu hiyo Emery ambaye kwake mchezajj huyo anamuona kuwa na nafasi ya kawaida sana kama walivo wachezaji wengine wote katika klabu hiyo.

Ifahamike Ozil ndiye anayechukua malupulupu mengi ndani ya klabu hiyo kwa sasa lakini amekuwa hapewi kile anachostahili kupewa akiwa kama mchezaji wa kiwango cha juu vile. Juzi tu klabu yake ilipokea kichapo kutoka kwa West ham kitu ambacho kilionekana kuwachukiza mashabiki wengi kutokana na kutomwona mchezajj huyo akiwa uwanjani kuisaidia timu hiyo iweze kuondoka na alama kwenye mchezo huo.

Kwa sasa amekuwa na wakati mgumu kuendana na falsafa za mwalimu huyo huku akisema kwake yeye Ozil ni mchezaji wa kawaida kama walivyo wengine; kwa sababu kuna wakati anaisaidia timu na kuna wakati haisaidii yimu hiyo. Katika mazingira kwamba akiwa majeruhi au akiwa nje ya mchezo siku hiyo ni vigumu kwake kuisaidia timu; pia wakati mwingine mechi ikiwa upande wake anaweza kuipa msaada timu yake. Hivyo, kwake anampa nafasi kama wanayoipata wengine.

Uwezo wa mchezaji huanzia na namna mwalimu anavyomwamini mchezaji huyo katika wakati fulani, kama mchezaji atakosa kuaminiwa siku zote hupoteza ari ya kucheza soka katika yimu hiyo. Hayo kwa sasa yanaonekana kumtokea Ozil; kutokana na kuwa nje ya malengo ya mwalimu kwa sasa na kupewa nafasi finyu sana ndani ya klabu hiyo.

Sintofahamu za aina hii hupelekea wachezaji wengi kupotea kwenye ramani zao na mwishowe kuzihama klabu zao. Kwa umri wake bado ana nafasi ya kuudhihirishia ulimwengu kwamba ana makubwa ya kufanya ndani ya klabu yoyote anayoweza kusajiliwa. Maana bado ana soko la kusajiliwa popote pale na akadhihirisha thamani yake.

Tusishangae kumwona Ozil huyu akiihama klabu hii wakati wowote kama hali ndani ya klabu hiyo itaendelea katika hali ilivyo sasa kwake. Kutokana na hali kwamba, hawezi kuvumilia kuendelea kukalishwa benchi au kuwa kama mchezaji mbadala katika timu hiyo. Naye anaonesha dhahiri kwamba haipendi kabisa hali hiyo inayoendelea kwake.

Katika uongozi wa Wenger, Ozil alikuwa katika kikosi cha kwanza na alikuwa chaguo la kwanza kwenye mechi byingi akiwa na utimamu wa mchezo kwa siku hiyo. Kuna haja ya kumaliza tofauti hizo ili waweze kuisaidia klabu hiyo kufikia malengo na kuwapa mashabiki burudani wanayoitaka.

Acha ujumbe