Patrick Vieira - Nahodha mtukutu zaidi kwenye historia ya soka


Hakuna amabye hakuuona ubabe wake pale London stadium 2001, usiku ule arsenal ilipata ushindi mwepesi tu mbele ya West ham. Vieira alikula umeme baada ya kumchezea rafu mbaya sana Paul Di Canio. Wakati anatoka Neil Raddock alimfuata akimshinikiza atoke akikimbia, Vierra akamtemea mate. Polisi wawili waliingia kumkota atoke uwanjani mapema, mmoja aliishia juu ya kitanda cha hospitali.

Patrick Vieira

Vieira aliyekula umeme kabla hajaingia kuchukua nafasi ya mtu game ya Sunderland. Shabiki mmoja wa Sunderland alimuonesha kitendo cha ubaguzi wakati anapasha misuli moto, aliishia kuondoka uwanjani na pua iliyovunjika. Huyu ndiye Patrick Vierra asiyejua kuna sheria zinazoadhibu watenda maovu. Anajua kitu kimoja tu, sheria ni mkono wake, sheria ni maamuzi yake.

Agosti 14 mwaka 1996 alipokelewa pale Highburry akitokea Millan, dimba la nyumbani la Arsenal. Aliitoa sababu moja iliyomshawishi kujiunga na Arsenal. Alikuja kuzungumza kifaransa na Wenger. Alidhani maisha yangekuwa mepesi kuwa chini ya usimamizi wa mtu wa nyumbani.

Patrick Vieira, binadamu bora zaidi kuwahi kutokea Arsenal kwenye dimba la chini. Ukabaji wake wa kikatili, mapafu ya farasi na nguvu kwenye mwili wake wa kibantu, Arsene Wenger alimleta kufanya kazi zote za jalala kwenye dimba lake. Huku nyuma Vierra kuna Ljunberg, Gilberto na Pires . Haki alikuwa na mafu ya mbwa na alikuwa anatembea na mpira kutoka goli la timu yake mpaka goli la timu pinzani.

Alikabidhiwa kitambaa cha unahodha May 2002, maneno machache ninayoyakumbuka kutoka kwake, “haya ni majukumu mapya ninayoyafurahia, ili uwe nahodha bora unatakiwa kuwa mfano kwa wengine, ninaahidi nitabadilika na kuacha utukutu”. Wiki moja baadae alikula umeme game ya Chelsea baada ya rafu mbaya kwa GianFraco Zola.

Acha ujumbe