Ricardo Kaka na Miujiza Yake Katika Soka la Kimataifa

Miaka 12 iliyopita, usiku mmoja wa baridi kali pale Paris Ufaransa, pale Seip Blatter aliposhika mic na kuitangazia dunia kuwa Ricardo Kaka ndiye mchezaji bora wa dunia wa mwaka 2007. Ninakumbuka maneno haya machache yaliyobeba uzito wa hotuba yake. “Ndoto zangu zilikuwa kucheza Sao Paolo tu na mechi moja kwa timu ya taifa ya Brazil, ila maandiko yanasema ukiomba madogo unapewa makubwa.”

Ninazikumbuka kelele za shangwe baada ya hapo za mashabiki 20,000 waliokuwa wameketi ndani ya Paris Opera House. Wengi wakilikumbuka bao lake la pili dhidi ya Mashetani wekundu pale theatre of dreams “old Trafford Manchester”. Namna alivouzima ule mpira kwenye chaki, namna alivondoka na ukuta mzima wa wanaume wanne wa United, namna alivouzungusha kwenda far post. Lile bao anafunga Ricardo Kaka tu. Nasema hivi! Lile bao anafunga Kaka tu!

Ila kama ilivokuwa tabia yangu ya kuwahi shule na kuacha daftari nyumbani, ili tu nirudishwe nyumbani, acha nikurudishe nyuma mpaka pale mjini Gama Federal, nchini Brazil alipozaliwa Kaka. Ardhi iliyotukuta kwa kuzalisha miungu ya soka kama Jair Ventura Filho ” Jairzinho”, Carlos Alberto, Eduardo Tostao mpaka kwa Carlos Verri Dunga “captain Dunga”. Ricardo Kaka alizaliwa huko na kupewa jina la Ricardo Izecscon dos Santos Leite. Ila mdogo wake alishindwa kulitamka, akalitamka kama “Caca”. Likazoeleka sana, Kaka akaamua kulifanya jina lake halali.

KAKA


Familia yake ililazimika kuhamia Sao Paolo akiwa na umri wa miaka 8,ili aende kujaribu kucheza soka katika klabu ya Sao Paolo. Alipofika kocha wa timu ya vijana ya Sao Paolo alimtazama kwa dakika moja tu, kisha akampa jezi namba 15. Hakuhitaji kumfanyia majaribio mtoto mwenye uwezo wa kuuchezea mpira namna ile.

Aliiona Jezi ya Sao Paolo ya wakubwa february 2001. Akaiongoza Sao Paolo kutwaa ubingwa wa kwanza na wa mwisho wa ligi ya miji Brazil. Msimu wake wa pili na Sao Paolo alifanya maajabu zaidi ya ule wa kwanza. Maajabu zaidi ya yale ya Kunar Newal wa India ya kuingia kwenye mdomo wa mamba na kutoka hai. AC Millan wakasema msituchezee, huyo aje Ulaya.

6 Komentara

    Mlokole aliyejua kulitandaza kabumbu safi

    Jibu

    Bonge la historia ana kipaji

    Jibu

    Kiajana mpole uwanjani ila maajabu yake makubwa!!!!!

    Jibu

    kaka mtu mbayaaah

    Jibu

    Brazil na Argentina Soka kwao ni zaidi ya burudani, ni Dini na kuna waumini wengi sana wa Dini soka ktk nchi hizi. Nilipenda mno nidhamu yake ktk mchezo wa soka#meridianbettz

    Jibu

    Unaweza sema kaka amezariwa na kipaji chake toka tumboni

    Jibu

Acha ujumbe