Sajili za Januari Zilizovunja Rekodi

Inapokaribia Januari kunakuwa na maingizo mapya katika vikosi vya timu mbalimbali. Yafuatayo ni baadhi ya majina ya wachezaji yaliyowahi kusajiliwa Januari [kipindi cha nyuma] na kufanya vizuri sana katika ngazi ya klabu.

Arsenal , aliyewahi kuwa mchezaji wa klabu hiyo Theo Walcott ambaye kwa sasa anakipiga na Everton ni miongoni mwa usajili wa awali kabisa wa mwezi Januari ambapo alijiunga na klabu hiyo akiwa na umri wa miaka 16 hii ilikuwa ni mwaka 2006; na amekuja kuondoka klabuni hapo akiwa na miaka 28. Amecheza mechi 397: akifunga magoli 108 huku akishinda makombe manne. Ameichezea Arsenal mechi nyingi katika historia zaidi ya Thiery Henry.

Chelsea, kuwasili kwa wachezaji kama Kevin de Bruyne (2012) na Mohamed Salah (2014) kulionesha kuwafanya Chelsea kama watawala wa soka la Uingereza; pia kwa kuongeza kumsajili Gary Cahill mwaka 2012. Usajili wa Mserbia Branislav Ivanovic uliibua mapya mengi na kuifanya klabu hiyo kuwa na kikosi kipana mchezaji huyu ameitumikia klabu hiyo kwa miaka nane akishinda vikombe kumi darajani hapo.

Leicester City, kuna wachezaji kama Riyard Mahrez akisaini mkataba kutoka Le Havre; na akabahatika kuchukua tuzo ya mchezaji wa mwaka katika ligi ya Uingereza amayo aliipata ndani ya misimu miwili. Wachezaji wengine ni Wes Morgan na Drinkwater ambao walisajiliwa mwaka 2012 ambapo wamedumu na timu hiyo kwa miaka 7 hadi sasa.

Liverpool, uwepo wa Luis Suarez katika kikosi cha majogoo ulikuwa ni wa msingi na wenye faida sana akiwa kama sehemu ya usajili wa Januari: japo baadae alitimkia Hispania. Kwa sasa anaweza kusahaulika kutokana na uwepo wa Van Dijk kikosini hapo ambaye amekuwa msaada mkubwa sana. Kwa sasa anapoteza nafasi hiyo ya kubeba historia ya mchezaji aliyasajiliwa Mwezi Januari kwa kuwepo wengine kama Philippe Coutinho, Daniel Sturridge, Maxi Rodriguez, Javier Mascherano, Daniel Agger na Steven Caulker. Amefunga magoli 69 kati ya mechi 110 katika ligi ya Uingereza.

Manchester City, usajili wao uliopata kuvunja rekodi ulikuwa na wachezaji kama Eden Dzeko. Alikuwa na msimu mzuri sana ambapo alimshawishi hata Mourinho kumzungumzia kwamba kwa mwaka 2014 alistahili kupata tuzo ya mchezaji wa mwaka kwa ligi ya Uingereza. Aliifungia klabu yake magoli 50 kati ya michezo 130  ya ligi hiyo, ambapo ni michezo 74 aliyoanza.

Manchester United, Patrice Evra ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa Januari na kuonesha umuhimu kikosini hapo. Akiwa kama beki wa kushoto; Mfaransa huyo alikuwa hapitiki kizembe wakati wa kushambuliwa akiwa na klabu hiyo.

Hao ni baadhi tu wachezaji waliosajiliwa mwanzoni mwa mwaka kwa baadhi ya timu zinazosumbua kwenye ligi hiyo. Tusubiri kuona sajili nyingine za Januari, kwa sababu inasemekana nyingi huwa imara sana kwa sababu kila timu husajili kuziba mapungufu.

Acha ujumbe