Liverpool wameendeleza rekodi yao ya ushindi katika Ligi Kuu ya Uingereza kwa kuibuka na ushindi wa bao 1–0 dhidi ya Burnley, kwenye mchezo uliochezwa ugenini katika uwanja wa Turf Moor. Ushindi huo wa nne mfululizo unawafanya The Reds kufikisha pointi 12, na kuendelea kukalia kilele cha msimamo wa ligi kuu Uingereza.
Mchezo huo uliokua wa kasi, huku Liverpool wakimiliki mpira kwa asilimia kubwa lakini wakikumbana na ukuta mgumu wa Burnley. Kikosi cha Arne Slot kilijaribu mipango tofauti kuvunja ngome ya Burnley huku nyota wapya kama Ekitike na Florian Wirtz wakijaribu kutafuta mianya ya kufunga.
Licha ya mashambulizi ya mara kwa mara, Burnley walijipanga kwa nidhamu ya hali ya juu, wakizuia mashambulizi hayo na hali ya mchezo ilibaki kuwa ya kusuasua hadi dakika za majeruhi, ambapo presha ya wapinzani ilizaa matunda kwani Oguchuku alipewa kadi nyekundu na kuwaacha Burnley wakiwa pungufu uwanjani.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Katika dakika ya 95, mpira ulipigwa na kuonekana kugusa mkono wa Hannibal Mejbri wa Burnley ndani ya eneo la hatari hivyo kuwapa mkwaju wa penalti Liverpool. Mohamed Salah alichukua jukumu hilo kwa utulivu wa hali ya juu, na kutuma mkwaju mkali uliomzidi kipa wa Burnley, kuwapa Liverpool bao pekee na la ushindi kwenye mchezo huo.
Burnley, licha ya kupoteza, walionyesha ukomavu wa kiuchezaji kwa kuhimili presha ya timu kubwa. Hata hivyo, kosa moja la kiufundi limewafanya waondoke bila pointi, jambo ambalo linaweza kuwa somo kwa mechi zijazo.
Kwa sasa, Liverpool wanaonekana kuwa na kasi ya kuendelea kutetea ubingwa msimu huu na mashabiki wa The Reds wana kila sababu ya kutabasamu, huku Salah akiendelea kuwa muhimili wa ushindi kwa Liverpool.