Mara baada ya Sun kuripoti kuwa meneja wa klabu ya soka ya Manchester City, Pep Guardiola amempa onyo winga Leroy Sane akitaka asipoteze mwelekeo wake nao Daily Star wanaripoti kuwa Manchester City watasubiri kwanza kabla ya kumpa ofa mpya mchezaji kiungo wa kati Phil Foden.
Foden anatarajiwa kusaini mkataba mpya wa muda wa miaka mitano wa dau la paundi 250,000 kwa juma na pia meneja amekataa uzushi wa kuwa anataka kumnasa mchezaji mshambuliaji Kylian Mbappe wa Paris Saint-Germain.
City na wengine wanamuwinda Mserbia
Daily Mirror wanaripoti kuwa mawakala wa klabu ya soka ya Manchester City, Liverpool na Tottenham walimuangalia kiungo wa kati wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic wakati akikipiga kwenye gemu iliyowapa ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Genoa wikiendi iliyopita. Ila sasa Mserbia huyo ameongezewa mkataba wa miaka 5 na klabu yake!


Povel
Gud news
Issa
City wakiamua usajil wanafanya