Ligi kuu ya Scotland ‘Scottish Professional Football League (SPFL)’ wamepanga kuanza kutumia Video Assistant Referee VAR kabla ya mwaka huu kuisha ikiwa tu vilabu binavyoshiriki kwenye ligi hiyo wataamua kupiga Kura ya kupitisha mfumo.
Scottish Professional Football League (SPFL) na vilabu vyake vinavyoshiriki ligi hiyo, kuwa zoezi la kupiga kura ili kuruhusu mfumo huo kufanya kazi litafanyika 19 April, likifanikiwa kupitishwa utekelazaji wake utaanza baada ya kombe la dunia kuisha.
Ili mdumo wa matumizi ya VAR uweze kupitishwa inahitajika 75% za kura kutoka kwenye Premiership clubs, 75% ya kura kutoka Championship na 75% ya kura kutoka kwenye vilabu vya League 1 na 2 kwa pamoja. Vilabu vyote 42 SPFL vitapiga jura kwenye swala hilo tu, wakati gharama zitachangiwa na vilabu vya Premiership clubs.
Gharama za mafunzo ya VAR zitasimamiwa na chama cha soka cha nchini humo Scottish FA ili kuwapa uzoefu na mifumo inayotumiwa kwenye michezo ya kimataifa na mashindano ya ulaya.
“Kutakuwa na zoezi la kupiga kura 19 April ikiwa tunahitaji kuweza kuruhusu matumizi ya VAR kwenye ligi zetu,” waraka wa SPFL.
“Ikiwa zoezi hili litafanikiwa, basi utekelezaji wake utaanza baada ya kukamiliki kwa mashindano ya kombe la dunia.”
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.