Simba wa Teranga, Senegal, Watinga Nusu Fainali Mbele Ya Mali

Senegal imeandika historia nyingine kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 baada ya kuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya nusu fainali, ikipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Mali katika Uwanja wa Grand Tangier. Mchezo huo uliokuwa wa presha kubwa ulidhihirisha uzoefu na ukomavu wa Simba wa Teranga, waliocheza kwa nidhamu ya hali ya juu hadi filimbi ya mwisho.

Dakika za mwanzo zilishuhudia mchezo wa tahadhari kutoka pande zote mbili, kila timu ikisoma mbinu za mpinzani wake. Mali walionekana kuwa na kasi kidogo walipojaribu bahati yao kwa shuti kali la Nathan Gassama, lakini ngome ya Senegal ilisimama imara kuzuia hatari hiyo mapema.

Simba wa Teranga, Senegal, Watinga Nusu Fainali Mbele Ya Mali

Tofauti ya mchezo ilikuja kupitia Iliman Ndiaye, ambaye alitumia vyema makosa madogo ndani ya eneo la hatari la Mali. Akiwa makini na mwenye utulivu, Ndiaye aliunganisha mpira kwa kuupiga kwa chini, bao lililowapa Senegal uongozi na kuwapa morali kubwa kabla ya mapumziko.

Bila kusahauΒ meridianbetΒ ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Mali walipata pigo kubwa zaidi kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika baada ya kiungo wao muhimu, Yves Bissouma, kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje. Tukio hilo lilibadilisha mwelekeo wa mchezo, kwani Senegal waliinufaika na idadi kubwa ya wachezaji na kuanza kudhibiti tempo ya mechi.

Simba wa Teranga, Senegal, Watinga Nusu Fainali Mbele Ya Mali

Kipindi cha pili kilikuwa cha usimamizi na subira kwa Senegal, wakilinda bao lao huku wakitafuta nafasi za kuongeza ushindi. Ingawa Mali walipata nafasi moja hatari iliyookolewa kwa ustadi na Edouard Mendy, Simba wa Teranga walidhibiti hadi mwisho na kuhakikisha tiketi ya nusu fainali. Sasa macho yao yanaelekezwa kwenye pambano lijalo dhidi ya ama Misri au Ivory Coast, wakisaka hatua moja zaidi kuelekea taji la Afrika.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.