Wakati ambapo kuna ripoti za klabu ya soka ya Barcelona kuwa ina uwezekano wa kumtoa Ivan Rakitic ili imsajili mpiga soka wa kimataifa wa huko Italia, Marco Verratti anayekipiga pale PSG, kumekuwa na habari kwamba kocha mkuu mpya wa klabu hiyo, Ernesto Valverde ametoa madai kwamba yeye hana wasiwasi na kikosi chake cha sasa!
Amefunguka na kusema kuwa itakuwa safi sana endapo wakisaini wasakata kabumbu wapya lakini yeye ana furaha sana kufanya kazi na wale waliopo klabuni hapo.
Kwa mujibu wa ripoti ya huko Hispania ilidai kuwa klabu ya Barcelona ipo tayari kumtoa Rakitic pamoja na kitita cha euro milioni 65 kwa PSG ili wamnase Verratti na hata hivyo Valverde akasisitiza kuwa wote wawili, Rakitic na Gomes, bado wanatakiwa pale Nou Camp na wamo kwenye mipango yake.
Shafii
Good news