Hali ya sintofahamu imeendelea kutawala kwa familia na wapenzi wa mwanasoka aliyekuwa akikipiga kwenye klabu ya Nantes, Emiliano Sala (28). Kutoweka kwake kunaumiza vichwa polisi kubaini mahali ambapo anaweza kuonekana kwa sasa.
Nyota huyu alitoweka kwenye ndege binafsi iliyopoteza mawasiliano akiwa safarini kutokea Nantes kwenda Cardif ambako alikuwa anatarajia kuanza majukumu yake mapya. Mawasiliano ya ndege hii yanaripotiwa kupotea karibu na visiwa vya Channel. Sala ana asili ya Argentina na amekulia Ufaransa anacheza nafasi ya kiungo wa katikati.
Kuna wasiwasi mkubwa kama nyota huyu, na mwenziye waliyekuwa naye kwenye ndege hiyo watakua hai mpaka sasa ikiwa waliangukia majini. Jitihada za kuwatafuta katika sehemu ambayo mawasiliano yao yalipotea bado zinaendelea. Lakini pia kuna tumaini kuwa huenda nyota huyu na mweziye wakawa hai kutokana dalili zinazo onekana baada ya kuwakosa eneo la bahari ambalo walipotea kwenye rada karibu na Channel Islands.
Kabla ya kupoteza mawasiliano kabisa, Sala anaripotiwa kuwa alituma ujumbe kuwa alikuwa kwenye ndege ambayo inaonekana kupoteza muelekeo, na alikuwa anaogopa sana. Dhana za polisi zimeangazia sehemu 4 na kuweka kipaumbele kwenye dhana kuwa nyota huyu na mwenziye watakuwa hai.
“Nipo kwenye ndege. Inaonekana kama inaanguka, Kama ndani ya saa moja na nusu hamtasikia chochote kutoka kwangu, sifahamu kama watamuagiza yeyote kuja kunichukua kwa sababu hawataweza kuniona…. naogopa” -Ujumbe wa mwisho wa Emiliano Sala kabla ya kupotea.
Mashabiki wake wa Nantes, wamekuwa wakitoa heshima zao wakiwa na hofu kama hatakuwa hai, lakini wanapata tumaini kidogo sana la uwezekano wa kupatikana akiwa mzima.
Sala alianza kujihusisha na soka akiwa katika klabu ya vijana ya San de Progreso (1994-2005) kisha Proyecto Crecer (2005-2010). Baada ya hapo nyota huyu akajiunga na kikosi kikubwa cha Proyecto Crecer mwaka huo 2010. Amechezea klabu zingine za; G. Bordeaux, US Orlrans, FC Niort, SM Caen, FC Nantes.


Issa
Emiliano sala dah imebaki majonzi tu
Povel
Rip salah