Kocha aliyeipatia mafanikio makubwa sana katika soka kwa kuipa vikombe vingi na kuzalisha wachezaji wenye kariba ya pekee duniani, Sir. Alex ameamua kuacha kuugulia maumivu ya ndani kutokana na timu yake ya zamani kufanya vibaya kwenye ligi kwa kurudi klabuni hapo akiwa kama mshauri wa masuala ya kisoka; wakiwa na lengo kubwa la kuirudisha timu hiyo kwenye ramani.

Mkongwe huyo ameshiriki katika mchakato mzima wa kumpata kocha aliyeishikilia kwa muda timu hiyo; ili waweze kurejesha hadhi yao waliyokuwa nayo kwenye misimu ya nyuma. Baada ya kutimuliwa klabuni hapo aliyekuwa kocha wao; Fergie, alisaidiana na viongozi wa juu wa klabu hiyo katika kushauri nani apewe timu hiyo ili kuinusuru na aibu zaidi. Amejaribu hata kumrejesha aliyekuwa msaidizi wake enzi zake anaefahamika kama Mike Phelan ili asaidiane kazi na kocha wa sasa, Ole.

Na kwa taarifa zinazoendelea ndani ya klabu hiyo ni kwamba, aliyewahi kuwa mlinda mlango wa timu hiyo Peter Schmeichel anatazamiwa kurejea klabuni hapo akiwa kama Mkurugenzi  wa soka katika ngazi ya klabu, kukiwa na lengo kubwa la kuleta ushindani kwa nafasi waliyonayo na kuthamini mchango wao ndani ya viunga hivyo walivyokuwepo.

Mkurugenzi msaidizi, Ed Woodward hakuwa na namna kwa kuamua kumrudia Fergie kuomba usaidizi wake baada ya kushindwa kufanya vizuri na makocha watatu ndani ya kipindi kifupi. Hili alilifanya baada ya kumtimua Mourinho kutokana na mwenendo wake ndani ya klabu hiyo. Ikumbukwe wakati wa uteuzi wa Mourinho, mkurugenzi huyu hakushirikisha mtu yeyote kati ya wakongwe hao kitu ambacho anajiona kama alifanya makosa makubwa sana kwa kushindwa kufanya hivyo, akaamini inaweza kuwa ni sababu iliyomfanya kukosa mtu anateendana na falsafa ya timu hiyo.

Sio Fergie peke yake anaisaidia kimawazo bodi ya timu hiyo pia kuna watu wengine kama Scot, Bobby Charlton na David Gill wanamchango mkubwa katika kuishauri timu hiyo kwa namna moja au nyingine: wakiwa kama watu waliojenga historia ndani ya klabu hiyo hadi leo hii.

Hatua hiyo ya kutaka kufanya kazi na wakongwe waliohudumu na timu hiyo awali, inakuja baada ya kuona wengi wanaoajiriwa kuchukua mikoba ndani ya timu hiyo wanashindwa kuendana na mifumo, kasi na mahitaji ya kila mmoja ndani ya klabu hiyo; kitu ambacho kinaipoteza historia nzuri iliyojengwa klabuni hapo.

3 MAONI

  1. wanashindwa kuendana na mifumo, kasi na mahitaji ya kila mmoja ndani ya klabu hiyo; kitu ambacho kinaipoteza historia nzuri iliyojengwa klabuni hapo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa