Ancelotti Matatani Ndani ya Real Madrid

Kocha wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti yupo matatani ndani ya klabu hiyo kwasasa kutokana na matokeo ambayo sio mazuri ambayo klabu hiyo imekua ikiyapata siku za karibuni.

Ancelotti ambaye amefanikiwa kuipatia klabu ya Real Madrid mataji matatu msimu uliomalizika na msimu huu tayari ameshatwaa taji la Uefa Super Cup, Lakini amekaa kwenye kiti cha moto mpaka sasa kutokana na matokeo inayopata klabu hiyo kwasasa.ancelottiKlabu ya Real Madrid mpaka sasa imeachwa kwa alama 9 na mahasimu wao klabu ya Barcelona kwenye ligi kuu nchini Hispania, Imewafanya klabu ya Real Madrid kua kwenye hatihati ya kuutema ubingwa wa ligi kuu nchini Hispania mpaka sasa.

Kocha Ancelotti ameiongoza klabu hiyo kwa vipindi viwili tofauti na vipindi vyote amefanikiwa kuiongoza klabu hiyo kutwaa taji la ligi ya mabingwa barani ulaya, Lakini kwa kiwango cha msimu huu kinamuweka kocha huyo kwenye wasiwasi mkubwa kua huenda akaondolewa klabuni hapo.ancelottiVyanzo vya ndani vinaeleza kua kocha Ancelotti alihisi kutohitajika ndani ya klabu hiyo tangu mwanzoni mwa msimu, Kutokana na klabu hiyo kutompa sapoti ya kutosha katika usajili hivo kocha huyo anajua wazi kua akishindwa kushinda taji lolote msimu huu ataondolewa ndani ya timu hiyo.

Acha ujumbe