Ancelotti: Hatutasajili Januari

Kocha wa klabu ya Real Madrid raia wa kimataifa wa Italia Carlo Ancelotti maarufu kama Don Carlo ameweka wazi kua klabu hiyo haina mpango wa kuingia sokoni katika dirisha dogo la mwezi Januari.

Kocha Ancelotti ameweka wazi hawana mpango wa kuingia Januari sokoni jambo ambalo mashabiki wengi walikua wanatarajia klabu hiyo iingie sokoni kutokana na majeraha yanayoiandama klabu hiyo.ancelottiReal Madrid imekua ikiandamwa na majeraha kwa wachezaji wake muhimu kama golikipa Thibaut Courtois, beki Eder Millitao na wachzaji wengine ambao wamekua wakipata majeraha na kurudi uwanjani.

Klabu hiyo inatarajia kuwapokea wachezaji wake wawili Thibaut Courtois na Eder Millitao kabla ya msimu kuishi, Jambo ambalo limemfanya kocha Carlo Ancelotti kusema Jnauari wao hawataingia sokoni kufanya usajili wowote.ancelottiKlabu ya Real Madrid kutokuingia sokoni ni wazi wanaamini katika kikosi chao walichokua nacho mpaka sasa, Licha ya majeraha waliyokua nayo mpaka wakati na wanaamini wachezaji wao majeruhi watarejea kabla ya msimu kumalizika.

Acha ujumbe