Ancelotti: Nitabaki Madrid hata Baada ya Kua Kocha

Kocha wa klabu ya Real Madrid raia wa kimataifa wa Italia Carlo Ancelotti ameweka wazi ataendelea kusalia ndani ya klabu hiyo hata baada ya kumaliza kufundisha soka ndani ya klabu hiyo.

Kocha Ancelotti amesaini mkataba mpya ndani ya klabu ya Real Madrid ambapo atasalia ndani ya klabu hiyo mpaka 2026, Lakini kauli ya raia huyo wa kimataifa wa Italia inaonesha ana mpango wa kuendelea kua klabuni hapo kwa muda mrefu zaidi.ancelottiKocha huyo wa zamani wa Ac Milan amesema pia kua alifanya mazungumzo na shirikisho la soka la Brazil, Lakini ukweli ni kwamba akili yake ilikua inasubiria ofa ya klabu ya Real Madrid na sio sehemu nyingine yeyote.

Brazil wanaelezwa walikua wanamfatilia kwa karibu zaidi kocha huyo wakihitaji akaiongoze timu ya tiafa ya Brazil, Lakini mpaka sasa inaonekana dili hilo limegonga mwamba baada ya kocha huyo kusaini mkataba mpya na Real Madrid ambao utamuweka klabuni mpaka mwaka 2026.ancelottiKocha Carlo Ancelotti amekua hasiti kuweka wazi mapenzi yake juu ya klabu ya Real Madrid mbali na kua kocha wa klabu hiyo, Hivo jambo hilo ndo limefanya mpaka kocha huyo kufikiria kubaki ndani ya timu hiyo hata pale muda wake wa kufundisha utakapomalizika.

 

Acha ujumbe