Ancelotti Aikataa Brazil Tena

Kocha wa klabu ya Real Madrid raia wa kimataifa wa Italia Carlo Ancelotti ameonekana kukanusha tena habari zinazomuhusisha yeye kujiunga na timu ya taifa ya Brazil.

Ancelotti akifanya mazungumzo na wanahabari amesema anajisikia furaha kua kocha wa Real Madrid jambo ambalo linaendelea kuvunja matumaini ya mashabiki wa timu ya taifa ya Brazil ambao walitamani kocha huyo akinoe kikosi chao.ancelottiKocha huyo amekua akihusishwa na timu ya taifa ya Brazil kwa takribani mwaka sasa lakini mara zote majibu yake yamekua ni yaleyale kua ana furaha kuwepo ndani ya klabu ya Real Madrid na hana mpango wa kuondoka klabuni hapo.

Taarifa zinaeleza kua ni kweli chama cha soka cha Brazil kimemfuata mara kadhaa kocha huyo na kuhitaji achukue majukumu ya kukinoa kikosi chao, Lakini kocha huyo amekua akiiipa Real Madrid nafasi kubwa zaidi kuliko jambo lolote.ancelottiBaada ya kuikataa ofa ya chama cha soka nchini Brazil kocha Carlo Ancelotti alifanikiwa kusaini mkataba mpya ndani ya klabu ya Real Madrid, Hii ikimaanisha kocha huyo bado yupo sana kwenye viunga vya Santiago Bernabeu tofauti na ilivyodhaniwa awali kua huenda angetimka hivi karibuni.

Acha ujumbe