Ancelotti Matumaini Kibao La Liga na UCL

Kocha wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti ameonesha bado ana matumaini kurejea kwenye ubora wao kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya pamoja na ligi kuu nchini Hispani La liga.

Klabu ya Real Madrid haijafanikiwa kuanza msimu vizuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya pamoja na ligi kuu nchini Hispania La liga, Hivo kocha Ancelotti ameeleza wana uwezo wa kurejea kwenye ubora wao na kuanza kufanya vizuri kwenye michuano hiyo ambayo wameonekana hawako vizuri.Ancelotti“Tutapigania mataji yote, hakika.”

“Tuna Kombe la Mabara mwezi Desemba. Tutakazana katika La Liga. Tutarejea vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa.

Real Madrid ni wazi hawapo kwenye kiwango bora kwasasa ambacho mashabiki wa klabu hiyo wanakitambua lakini kocha Ancelotti ana matumaini kua watarejea kwenye ubora wao punde tu baada ya kumalizika kwa michuano ya klabu bingwa ya dunia ambayo watakwenda kucheza baada ya mapumziko ya michuano ya kimataifa.

Acha ujumbe