Ancelotti:Arda Guler Kurejea hivi karibuni

Kocha wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti amesema kiungo kinda wa klabu hiyo Arda Guler atarejea uwanjani hivi karibuni baada ya kutoka kwenye majeraha ambayo aliyapata.

Kinda Arda Guler alikua akiandamwa na majeraha tangu atue klabuni hapo akitokea klabu ya Fenerbahce ya nchini kwao Uturuki, Lakini Ancelotti anasema kiungo huyo ataonekana hivi karibuni akitinga jezi ya Real Madrid.ancelottiKiungo huyo kinda mwenye kipaji kikubwa alipata majeraha wakati klabu hiyo ikijiandaa na msimu mpya nchini Marekani, Lakini siku kadhaa nyuma aliripotiwa kupona majeraha kabla ya kupata majeraha mengine kwenye mazoezi.

Kocha Ancelotti anasema mchezaji anataka kuja kwa namna ya tofauti huku akisisitiza ni kijana mdogo, Hivo ana muda mwingi wa kuonesha ubora wake ndani ya klabu hiyo ikiwa inaonesha klabu haina haraka ya kumrudisha uwanjani.ancelottiArda Guler kijana mwenye miaka 18 Real Madrid wanataka kukitunza kipaji hichi na kwenda nacho taratibu na ndio sababu kubwa ya kocha wake kusema anaingia taratibu kwenye timu wakimtaka apone majeraha yake kabisa ili akianza kucheza kusiwe na hofu yeyote.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.