Araujo Arejea Mazoezini Barca

Beki wa klabu ya Fc Barcelona raia wa kimataifa wa Uruguay Ronald Araujo inaelezwa amerejea mazoezini baada ya kusumbuliwa na majeraha ya muda mrefu yaliyomuweka nje kuanzia mwezi wa saba mpaka sasa.

Araujo anarejea ndani ya kikosi cha Barcelona wakati sahihi sana kwani klabu hiyo kwasasa inapitia kipindi kigumu kutokana na majeraha ambayo yamekua yakiisibu klabu hiyo haswa kwenye eneo la ulinzi, Hivo beki huyo wa kimataifa wa Uruguay akianza kuitumikia klabu hiyo litakua jambo muhimu sana.araujoBeki huyo mwandamizi klabuni hapo amekua kwenye kiwango bora sana kwa misimu miwili iliyopita hivo kukosekana kwake ndani ya klabu hiyo imekua pigo, Japokua kocha Flick alitengeneza safu nzuri ya ulinzi ambayo imecheza kwa kuelewana sana kwa kipindi hichi ambacho beki huyo hakuepo.

Kurejea kwa beki Araujo ni taarifa njema sana kwa mashabiki wa klabu ya Barcelona lakini pia kwa benchi la ufundi la klabu hiyo likiongozwa na kocha Hans Flick, Kwani atakwenda kuongeza ubora kwenye safu ya ulinzi ya klabu hiyo haswa kipindi hichi ambacho beki Balde amepata majeraha.

Acha ujumbe