Arbeloa Akubali Hasira za Mashabiki Baada ya Barcelona Kutwaa LaLiga

Kocha wa Real Madrid, Alvaro Arbeloa, amesema klabu hiyo inaelewa hasira na maumivu ya mashabiki wake baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa FC Barcelona katika mchezo wa El Clasico uliowafanya wapinzani wao kutwaa rasmi ubingwa wa LaLiga.

Arbeloa Akubali Hasira za Mashabiki Baada ya Barcelona Kutwaa LaLiga Kipigo hicho kilihitimisha msimu mbaya kwa Real Madrid ambao wamemaliza bila taji lolote, huku Barcelona wakitwaa ubingwa wao wa 29 wa LaLiga wakiwa wamebakiza michezo mitatu. Madrid pia walitolewa kwenye hatua ya robo fainali ya UEFA Champions League na Bayern Munich, jambo lililoongeza presha ndani ya klabu hiyo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Akizungumza baada ya mchezo huo, Arbeloa alisema “Hakuna mengi ya kusema. Tunaelewa hasira zao, maumivu yao na namna walivyokatishwa tamaa na msimu huu. Tunachoweza kufanya ni kufanya kazi kwa bidii na kujifunza kutokana na makosa yote tuliyofanya mwaka huu.”

Arbeloa Akubali Hasira za Mashabiki Baada ya Barcelona Kutwaa LaLiga Kocha huyo pia alisisitiza kuwa Real Madrid ni klabu yenye historia ya kurejea kwa nguvu hata baada ya vipindi vigumu. “Real Madrid imewahi kuanguka mara nyingi na kurejea tena. Ninaelewa kabisa hasira za mashabiki, lakini lazima tufanye kazi kubwa kubadilisha hali hii,” alisema Arbeloa.

Arbeloa Akubali Hasira za Mashabiki Baada ya Barcelona Kutwaa LaLiga Wakati huo huo, hali ndani ya kikosi hicho imeonekana kuwa tete zaidi baada ya taarifa kueleza kuwa nahodha Federico Valverde alikimbizwa hospitalini kufuatia ugomvi wa vyumbani na kiungo Aurelien Tchouameni. Aidha, klabu hiyo pia ilimfuta kazi aliyekuwa kocha mkuu Xabi Alonso katikati ya msimu kutokana na matokeo mabaya.

Arbeloa Akubali Hasira za Mashabiki Baada ya Barcelona Kutwaa LaLiga

Licha ya mbio za ubingwa kumalizika, Arbeloa amesema wachezaji wake wanapaswa kuendelea kupambana katika michezo mitatu iliyobaki. “Tunaitetea nembo kubwa kuliko sisi wenyewe, ambayo ni nembo ya Real Madrid. Lazima tucheze kwa ushindani mkubwa na kuhakikisha tunashinda michezo iliyobaki,” aliongeza. Pia aliweka wazi kuwa mustakabali wake ndani ya klabu hiyo utaamuliwa baada ya msimu kumalizika.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.