Kocha wa Real Madrid, Alvaro Arbeloa, amethibitisha kuwa ataondoka kwenye nafasi yake mwishoni mwa msimu huu baada ya timu hiyo kumaliza bila kutwaa taji lolote.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Ijumaa, Arbeloa alikiri wazi kuwa hatakuwa kocha wa timu hiyo msimu ujao huku taarifa zikieleza kuwa kocha mkongwe Jose Mourinho anatarajiwa kurejea kuinoa klabu hiyo ya Hispania.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Real Madrid itashuka dimbani Jumamosi dhidi ya Athletic Bilbao katika mchezo wao wa mwisho wa La Liga utakaochezwa kwenye dimba la Santiago Bernabeu baada ya msimu wenye misukosuko mingi.
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez, alimpa Arbeloa nafasi ya kuinoa timu hiyo Januari baada ya kuondoka kwa Xabi Alonso, lakini sasa kocha huyo wa zamani wa Madrid anatarajiwa kuondoka na nafasi yake kuchukuliwa na Mourinho.

“Ndiyo,” alisema Arbeloa alipoulizwa kama ataondoka mwishoni mwa msimu huu.“Mournho ana benchi bora la ufundi na watu wazuri wanaomzunguka, hivyo kama atakuja Madrid atakuja na timu yake. Hakuna nafasi ya mimi kufanya kazi naye.”
Arbeloa, aliyewahi kuitumikia Real Madrid kati ya mwaka 2009 hadi 2016 kabla ya kuendelea kufundisha katika ngazi za vijana, alisema ana matumaini kuwa huu si mwisho wake kabisa ndani ya klabu hiyo.
“Natumaini hii si kwaheri bali ni tutaonana baadaye. Madrid imekuwa nyumbani kwangu kwa miaka 20 katika majukumu tofauti. Huu utakuwa mchezo wangu wa mwisho msimu huu kama kocha wa Real Madrid, lakini sijui kama utakuwa wa mwisho kabisa katika maisha yangu hapa. Nitajaribu kuufurahia na kuhakikisha tunapata ushindi.”


