Arda Guler Arejea Mazoezini Madrid

Kiungo kinda wa klabu ya Real Madrid raia wa kimataifa wa Uturuki Arda Guler ameonekana mazoezini klabuni hapo baada ya kupata majeraha wiki kadhaa zilizopita.

Arda Guler inaelezwa kua atakua timamu kwajili ya kurejea uwanjani baada ya michuano ya kimataifa kumalizika, Ikumbukwe mchezaji huyo bado hajafanikiwa kucheza mchezo wowote wa kimashindano klabuni hapo.arda gulerKiungo huyo wa kimataifa wa Uturuki mwenye kipaji kikubwa amekua akiandamwa na majeraha tangu atue klabuni hapo na kushindwa kucheza mchezo wowote tangu msimu huu umeanza.

Kiungo huyo ameshapata majeraha kwa vipindi viwili tofauti tangu ajiunge na timu hiyo kwa mara ya kwanza kwenye kipindi cha kujiandaa na msimu mpya, Huku majeraha mengine akiyapata wiki mbili zilizopita lakini kwasasa anaonekana yupo tayari kurejea uwanjani.arda gulerMashabiki wengi wa klabu ya Real Madrid wana hamu kubwa ya kumuona Arda Guler kiungo huyo kinda mwenye ufundi mkubwa, Ambapo wanatamani kuona ambavyo alikua akivifanya na klabu yake ya zamani ya Fenerbahce akivifanya ndani ya Real Madrid.

Acha ujumbe