Balde Apata Majeraha

Beki wa kushoto wa klabu ya Barcelona Alejandro Balde amepata majeraha katika mchezo wa ligi kuu ya Hispania leo na kushindwa kuendelea na mchezo huo ambao Barcelona wamepokea kichapo.

Beki Balde aliondolewa uwanjani na gari dogo la kubebea wagonjwa ikionekana ameshindwa kutembea ikiwa sio dalili nzuri kwake, Kwani inawezekana amepata majeraha makubwa ambayo yatamlazimisha kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kama ambavyo alisumbuliwa na majeraha msimu uliomalizika.baldeBado timu ya madaktari ya klabu ya Barcelona haijatoa taarifa rasmi kua mchezaji huyo atakaa nje kwa muda gani au amepata majeraha makubwa kiasi gani, Lakini haitajalisha kua atakaa kwa muda gani nje ya uwanja ila tayari litakua pengo kwa klabu hiyo kwani beki huyo amekua moja ya wachezaji muhimu klabuni hapo.

Beki Alejandro Balde msimu uliomalizika alisumbuliwa na majeraha ya muda mrefu ambapo alishindwa kuitumikia klabu hiyo kwa muda mrefu tofauti na msimu wa mwaka 2022/23, Lakini msimu huu ameonesha ubora mkubwa na kurejea kwake kumeiboresha Barca bahati mbaya kwake amepata majeraha tena ambayo pengine yanaweza kumuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Acha ujumbe