Barcelona na Madrid Wachuana kwa Kinda wa Kituruki

Vigogo wa soka kutoka nchini Hispania klabu ya Barcelona na klabu ya Real Madrid wameingia vitani kwajili ya kuinasa saini ya kinda wa kimataifa wa Uturuki fundi Arda Guler.

Kinda Arda Guler ambaye ana umri wa miaka 18 amewaingiza Vitani Barcelona na Real Madrid kutokana na ubora mkubwa ambao amekua akiuonesha kwenye klabu yake ya Fenerbahce kwenye msimu uliomalizka.BARCELONAKinda Arda Guler amekua akitolewa macho na vilabu kadhaa barani ulaya mbali na vilabu vya Barca na Madrid, Hii inatokana na maajabu ambayo amekua akionesha kiungo huyo licha ya umri mdogo ambao amekua nao.

Real Madrid wao wamekua wakisajili vijana wadogo miaka ya karibuni wakiwa na mipango ya kutengeneza timu bora kabisa miaka kadhaa mbele, Kwani mpaka sasa wameshajili wachezaji kama Vinicius Jr, Rodriygo, Jude Bellingham, Camavinga, na Endrick.BARCELONAKlabu ya Barcelona wao wanafahamika kwa namna wanavyotoa nafasi kwa vijana wadogo kuanzia kwenye timu yao ya vijana mpaka timu ya wakubwa, Hivo Arda Guler atakua kwenye mikono kadhaa akijiunga na timu yeyote kati ya hizo kwani zote zimeonesha namna ambavyo wanaweza kutoa nafasi kwa vijana wadogo.

Acha ujumbe