Barcelona Kummfukuzia Cancelo

Klabu ya Barcelona ipo kwenye mkakati wa kumnasa beki wa kulia wa klabu ya Manchester City raia wa kimataifa wa Ureno Joao Cancelo ambaye anataka kutimka klabuni hapo.

Barcelona wanaarifiwa wanasubiri dili la winga wao Ousmane Dembele ambaye anatimkia klabu ya PSG kukamilika, Hivo baada ya hapo watakua wameongeza kiasi cha pesa ambacho kitaweza kuwasaidia kukamilisha usajili wa beki huyo.BarcelonaKlabu ya Manchester City wako tayari kumuuza beki Joao Cancelo kama watapokea ofa ambayo inastahili kwa beki huyo kwani tangu mwanzo ameonesha ana nia ya kutimka ndani ya kikosi cha mabingwa hao wa ulaya na Uingereza.

Cancelo alitolewa kwa mkopo Januari kuelekea klabu ya Bayern Munich na mabingwa hao wa Ujerumani walikua wanahitaji kubaki nae, Lakini kiwango kikubwa cha pesa ambacho kimewekwa na Man City ndio kimewarudisha nyuma.BarcelonaBarcelona wao wanaona wanaweza kutoa dau ambalo klabu ya Man City wataridhia kwani wanatarajia kupokea kiwango kizuri cha pesa kwa klabu ya PSG ambao wako mbioni kumalizana na winga wa klabu hiyo Ousmane Dembele raia wa kimataifa wa Ufaransa.

Acha ujumbe