Klabu ya Barcelona imeweka wazi haitaingia sokoni katika diriaha dogo la mwezi Januari kwajili ya kuzipa pengo la kiungo wake Gavi ambaye amepata majeraha ya muda mrefu.
Rais wa klabu ya Barcelona Joan Laporta ameweka wazi hawatasajili katika dirisha dogo la mwezi Januari,Kwani wana kikosi kipana ambacho kina uwezo bado wa kuendelea kupambana.Rais Laporta ameongea hayo baada ya kuulizwa juu ya mustakabali wao wa kuingia sokoni kwajili ya Gavi ambaye atakua nje ya uwanja kwa muda mrefu ambapo Laporta ameweka wazi wana kikosi kipana.
Kiungo Gavi alipata majeraha siku kadhaa nyuma akiwa katika majukumu ya timu ya taifa ya Hispania, Ambapo majeraha hayo yanaelezwa yatamuweka nje ya uwanja kwa takribani miezi sita mpaka tisa.Kutokana na majeraha ya muda mrefu aliyoyapata Gavi ambaye ni moja ya wachezaji muhimu kabisa ndani ya kikosi cha Barcelona ilidhaniwa klabu hiyo itaingia sokoni Januari, Lakini majibu kutoka kwa Rais Laporta ni wazi klabu hiyo haitatafuta mbadala wa Gavi kwakua wana kikosi kipana.