Barcelona Kuipindua Liverpool kwa Amorim

Klabu ya Fc Barcelona inaelezwa inakaribia kuipindua klabu ya Liverpool katika kumuwania kocha wa klabu ya Sporting Lisbon ya Ureno Ruben Amorim ambaye anawaniwa na klabu ya Liverpool.

Barcelona mwishoni mwa msimu huu wataachana na kocha wake mkuu Xavi Hernandez, Hivo wako sokoni kutafuta kocha mkuu mwingine ambaye atakuja kuiongoza timu hiyo kuanzia msimu ujao na misimu mingine inayofauata.barcelonaJina la Ruben Amorim ni jina ambalo linatajwa sana kuchukua mikoba ya Xavi mwishoni mwa msimu, Lakini pia kocha huyo aanaelezwa kuwepo kwenye mawindo ya klabu ya Liverpool ili kuionoa timu hiyo baada ya Jurgen Klopp kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

Kocha huyo raia wa kimataifa wa Ureno amekua na msimu bora sana ndani ya klabu ya Sporting Lisbon, Jambo ambalo limefanya kuanza kufatiliwa na vilabu vikubwa barani ulaya kama Liverpool, Bayern Munich, Barcelona.barcelonaMabingwa watetezi wa ligi kuu ya Hispania klabu ya Barcelona mpaka sasa ndio wanaongoza kinyang’anyiro cha kumpata kocha Ruben Amorim ambaye alikua kwenye orodha fupi ya makocha waliokua wanatizamiwa kwa karibu kuchukua nafasi ya Jurgen Klopp.

Acha ujumbe