Barcelona Yadondosha Alama Tena

Klabu ya Fc Barcelona leo imedondosha alama tatu tena leo wakiwa nyumbani katika mchezo wa ligi kuu nchini Hispania dhidi ya klabu ya Las Palmas kwa mabao mawili kwa moja.

Barcelona leo wametimiza kucheza michezo mitatu mfululizo katika ligi kuu nchini Hispania bila kupata alama tatu muhimu, Kwani walipoteza mchezo wao dhidi ya Real Sociedad wakapata sare dhidi ya Celta Vigo wikiendi iliyomalizika na leo tena wamepoteza mbele ya Las Palmas na kutimiza michezo mitatu.

Klabu hiyo yenye maskani yake Catalunya inaonekana kujiweka kwenye presha kutokana na kudondosha alama kwani wapinzani wao klabu ya Real Madrid inaweza kuipiku Barca kama watashinda michezo yao miwili, Kwani mpaka sasa Barca wanaongoza kwa alama nne, Huku Madrid wakiwa na michezo miwili mkononi.

Mpaka sasa ligi kuu ya soka nchini Hispania inaonekana kuchangamka tofauti na ilivyoonekana mwanzo ambapo Barcelona walikua na fomu ya hali juu na wengi kuamini huenda wangekua mabingwa tena wakutangazwa mapema, Lakini mambo yamebadilika na sasa inonekana ubingwa bado hauna mwenyewe na yeyote anaweza kutwaa.

Acha ujumbe