Klabu ya Fc Barcelona itawakosa wachezaji wake wengi kuelekea mchezo wao dhidi ya klabu ya Real Madrid hatua ya nusu fainali ya kombe la Mflame nchini humo maarufu kama Copa de le Rey.

Klabu ya Barcelona itavaana na Real Madrid leo katika mchezo utakopigwa kwa mikondo miwili na mchezo wa kwanza leo unaanzaia katika dimba la Santiago Bernabeu, Huku Barca ikiwakosa wachezaji wake muhimu kama Roberto Lewandowski, Ousmane Dembele. Christinsen, pamoja Kiungo Pedri.barcelonaBarcelona ambao wametoka kutolewa kwenye michuano ya Uefa Europa na klabu ya Manchester United, Vilevile ikipoteza mchezo wake wa mwisho wa La liga itakua inaenda kukutana na Real Madrid ambayo inataka kulipiza kisasi dhidi ya miamba hiyo ya Catalans.

Wachezaji wa Barca wamekua wakiandamwa na majeraha mara kwa mara jambo ambalo limekua likiwakwamisha klabu hiyo pale ambapo wanakua wanawahitaji wachezaj wao kwenye baadhi ya michezo muhimu, Kama mchezo wa leo dhidi ya mahasimu wao klabu ya Real Madrid ni mchezo ambao walihitaji kua na wachezaji wao muhimu.barcelonaKlabu ya Real Madrid chini ya Carlo Ancelotti wameahidi kutokurudia makosa dhidi ya klabu ya Barcelona ambo wameonekana kuwasumbua sana Real Madrid siku za karibuni, Huku mara ya mwisho wakipoteza taji mbele ya Barca kwa kupoteza kwa mabao matatu kwa moja hivo mchezo wa leo ni kama kisasi kwa upande wao.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa