Uvumilivu umewashinda, FC Barcelona wameamua kuonesha ukubwa wa klabu kuliko mchezaji. Dembele rasmi, yupo sokoni Januari hii.
Kumekuwa na mvutano wa muda mrefu kuhusu suala la kusaini mkataba mpya kati ya Ousmane Dembele na Barcelona. Sakata hili lilianza toka kipindi cha Ronard Koeman na limeendelea hata wakati huu wa Xavi Hernandez.
Kiuhalisia, Dembele (pamoja na wakala wake) waliweka wazi kuwa, hakuna mkataba mpya utakaosainiwa na mchezaji huyo kwa matakwa ya klabu. Badala yake, yupo tayari kusaini mkataba mpya, endapo Barca watazingatia matakwa ya Dembele katika mkataba huo.
Picha zima lilibadilika baada ya Barca kuwasajili Dani Alves na Ferran Torres. Pia, kuongeza mikataba ya Pedri na Ansu Fati, Gerard Pique, Samuel Umtiti na sasa mchakato unaendelea kwa Gavi. Hii yote inamuonesha Dembele kuwa, Barca wanapesa na hivyo haoni kama ni sahihi yeye kupunguziwa mshahara katika mkataba ambao Barca wanataka kumsainisha.
Mapema wiki hii, wakala wa Dembele alisema wazi, wanachokifanya Barcelona (kutishia kumuondoa Dembele klabuni hapo kama hatosaini mkataba aliopewa ndani ya saa 48), ni kujichosha tu. Kwani, mchezaji pamoja na wakala wake, hawatishiki kwa lolote kutoka kwenye klabu hiyo.
Sasa ni rasmi, FC Barcelona imeamua kumuuza Dembele kwenye dirisha hili la Januari. Mkurugenzi wa Barca, Alemany amethibitisha kuwa;
Ni wazi kuwa Ousman Dembele hataki kuendelea kuwepo Barcelona. Hataki kuwa sehemu ya mipango yetu. Tumemwambia Dembele anatakiwa kuondoka sasa hivi. Tunategemea Ousmane atauzwa kabla ya Januari 31.
Dembele ameondolewa kwenye kikosi cha Barca kitakachocheza dhidi ya Athletico Bilbao leo usiku.
Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.
CHEZA HAPA