Barcelona Kuwaacha Waliowasijiri Dirisha Hili

Klabu ya Barcelona inampango wa kuwaacha wachezaji wake wawili ambao wamewasijiri kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi ambao ni Andreas Christensen na Franck Kessie bila ya kucheza mchezo wowote  kwenye klabu hiyo.

Andreas Christensen na Franck Kessie wamejiunga na Barcelona baada ya kuachana na klabu zao msimu huu mmoja akitokea Chelsea na mwingine akitokea  AC Milan. Tatizo la kifedha kwenye klabu ya Barcelona ndio chanzo cha kupunguzwa kwa wachezaji hao.

La Liga imewazuia klabu ya Barcelona kuwasijiri wachezaji kadhaa kwenye kikosi cha timu, mpaka waweze kuhakikisha kuwa wamewapunguza wachezaji au wameongeza mteji wa klabu hiyo.

Christensen na Kessie kwenye mikataba yao na klabu ya Barcelona kuna kipengere cha kuondoka huru kwenye viunga vya Camp Nuo, ikiwa hawatasajiri kwenye klabu hiyo kwa muda husika.

Pia wachezaji wengine ambao bado hawajasajiriwa ni Robert Lewandowski, Raphinha na Jules Koundé, japokuwa Sergi Roberto na Ousmane Dembélé wote wamesaini mikataba mpya lakini bado hawajasajiriwa baada ya mikataba yao ya awali kuisha.

Acha ujumbe