Klabu ya Barcelona imekanusha taarifa iliyotolewa na ARA kuwa Gerard Pique sakata lake la kutaka kupunguziwa mshahara halikuweza kufanikiwa kwa sababu ya klabu ilikuwa haina nia kumruhusu kununua hisa za umiliki wa klabu ya Barça Studios.

Mlinzi huyo wa kimataifa wa Hispania kuna taarifa zilitoka kuwa anavutiwa na kuhitaji kumiliki asilimia 24.5% za Barça Studios ambazo Barcelona walipanga kuziuza kwenye wimbi la nne ili kuweza kufufua uchumi wa klabu hiyo ili kuweza kusajiri wachezaji wapya.

Barcelona, Barcelona Wakanusha Pique Kutaka Kununua Barça Studios, Meridianbet

Pique alikuwa kwenye mazungumzo ya kupungumza mshahara wa kwenye klabu hiyo, lakini pia inasemekana kuwa alielezea nia yake ya kutaka kununua hisa za Barça Studios yeye mwenye lakini rais Joan Laporta akinktalia kwa sababu ni kinyume na maadili.

Taarifa zinaelezea zaidi kuwa maazungumzo ya makubaliano ya kimtakataba kati ya Pique na Barcelona yalishindikana. Japo klabu hiyo ilitoa waraka  rasmi kuhusu swala hilo, na kupinga shutuma zote zilizotolewa na ARA, na kusema hakuna mazungumzo ya taliofanyika kwenye hatua yoyote ya namna hiyo.

“Tumekutana na taarifa iliyochapishwa leo na gazeti la ARA likiwa na kichwa cha habari, Laporta amakatalia Pigue Barca Studio.

“klabu ya Barcelona inakanusha kwamba rais hakupokea offa yoyote kutoka kwa mchezaji wa kikosi cha kwanza Gerard Piqué wala kampuni yake kutaka kuchukua sehemu ya Barc studios.

“Klabu inasikitika kwa usambazaji wa taarifa zisizo na uthibitisho ambazo zinaweza kuharibu picha ya heshima ya wachezaji wa Barcelona.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa