Barcelona: Wanne Wabaki Mbio za Uraisi

Kuelekea Januari 24, 2021 – mbio za kuwania uraisi wa klabu ya Barcelona FC unashika kasi! Hii ni baada ya wagombea waliopita kwenye hatua ya kwanza kubaki wanne tu.

Mchakato wa kumpata raisi mpya wa klabu hiyo ulianza tangu 2020 kabla na baada ya raisi Bartomeu kujiuzulu nafasi yake ya kuiongoza Barcelona.

Victor Font

Kati ya majina ya wagombea waliotia nia ya kukamata usukani wa klabu hiyo ni Joan Laporta, Victor Font, Toni Freixa na Emili Rousaud waliosalia kwenye mchakato wa uchaguzi.

Kwa taratibu za uchaguzi, wagombea wote walipaswa kupata saini za wanaowasapoti huku idadi ya chini iliyowekwa ikiwa ni kura 2,257. Kwa idadi hiyo, Laporta amepata saini 10,272, Font (4,713), Freixa (2,822) na Rousaud (2,510).

Toni Freixa

Utaratibu wa kuhakiki saini hizi utafanyika leo (Jumanne) na matokeo ya watakaoidhinishwa yatatangazwa Alhamisi wiki hii.

Licha ya kuwa na mapendekezo ya kubadilisha tarehe ya uchaguzi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo COVID19, Barcelona wameendelea kusisitiza Januari 24 itabaki kama ilivyopangwa hii ni baada ya taratibu zote za uchaguzi kukubaliwa na mamlaka zote zinazohusika.

Emili Rousaud

Nani ataibuka kidedea kwenye kiti ya uraisi wa Barca? Atafanikiwa kumbakiza Leonel Messi au atamfungulia milango aondoke?? Kumekucha!!


MERIDIANBET INAKUPA NAFASI YA KUWA MILIONEA KWA KILA BAADA YA DAKIKA 5

Mchezo wa Keno unakupatia fursa ya kuibuka kidedea kupitia droo zinazochezwa kila baada ya dakika 5 tu!! Tunaposema Meridianbet ni nyumba ya mabingwa, tunamaanisha!!

INGIA MCHEZONI

16 Komentara

    Uchaguzi umepamba moto

    Jibu

    Kumenoga

    Jibu

    Ngoja tusubiri wakati ujibu

    Jibu

    Atariatari

    Jibu

    Tunamsubr mshnd

    Jibu

    Good news

    Jibu

    Uchaguzi unaendelea kupamba moto

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Asnt kwa taarif meridianbet

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Ngoja tuone

    Jibu

    Goodnews

    Jibu

    Atariii hapo

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Taarifa zimetulia

    Jibu

    pole yao

    Jibu

Acha ujumbe