Barcelona imefanikiwa kupata taji lao la kwanza la LaLiga tangu 2019 baada ya kuwafunga wapinzani wao wa jiji la Espanyol kwa mabao 4-2.
Sherehe hizo zilikatizwa, hata hivyo, wakati mashabiki wa Espanyol walipoingia uwanjani baada ya mechi huku wachezaji wa Barcelona wakinyanyua ushindi wao. Wachezaji walilazimika kukimbilia ndani ya vyumba vyao.
Robert Lewandowski alifunga mabao mawili kila upande wa Alejandro Balde dakika ya 20 kabla ya Jules Kounde kuongeza bao lao la nne baada ya muda wa mapumziko.
Javier Puado aliifungia Espanyol bao moja na Joselu akaongeza jingine dakika za lala salama, lakini ushindi huo unamaanisha kuwa Barcelona wanasalia na Real Madrid kwa pointi 14 kileleni ikiwa zimesalia mechi nne pekee kuchezwa.
Atletico Madrid walikosa nafasi ya kuwapita wapinzani wao Real Madrid katika nafasi ya pili baada ya kufungwa 1-0 na Elche walio mkiani mwa msimamo pale makosa ya kipa Ivo Grbic yalipomruhusu Fidel kufunga bao la kwanza kabla ya mapumziko.
Mabao matatu ya kipindi cha pili yalitosha kwa Sevilla kupata ushindi murua dhidi ya wapinzani wanaotatizika kushuka daraja Real Valladolid.
Rafa Mir aliwaweka wageni mbele na Papu Gomez akafunga bao lao la pili kabla ya Tecatito Corona, katika mechi yake ya kwanza tangu Agosti, kumaliza mchezo kwa bao la dakika za lala salama.
Alberto Mari alifunga bao la dakika za lala salama kwa Valencia na kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Celta Vigo.
Justin Kluivert aliweka wageni mbele kabla ya Haris Seferovic kusawazisha, lakini Mari akapata bao la ushindi kabla ya Gabriel Paulista wa Valencia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.