KLABU ya Barcelona inatajwa kupanga kufanya usajili mkubwa majira haya ya kiangazi kwa kuwania baadhi ya mastaa wakubwa wa soka barani Ulaya, huku mshambuliaji wa Atletico Madrid, Julian Alvarez, akiwekwa kwenye rada zao.
Taarifa zinaeleza kuwa Barcelona tayari imekubaliana dili la Euro milioni 80 la kumsajili Anthony Gordon kutoka Newcastle United, huku pia ikiendelea na mazungumzo ya kumpata Marcus Rashford moja kwa moja kutoka Manchester United.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kutokana na Barcelona kurejea kwenye sheria ya kifedha ya LaLiga ya 1:1, kocha Hansi Flick amepewa nafasi kubwa zaidi ya kufanya matumizi katika usajili wa wachezaji wapya kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao.
Kwa mujibu wa mwanahabari Fabrizio Romano, Barcelona tayari imetuma ofa ya Euro milioni 100 kwa Atletico Madrid kwa ajili ya kumtaka mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina, Julian Alvarez, ambaye pia anadaiwa kutamani kuondoka ndani ya klabu hiyo.
“Barcelona wametuma pendekezo la Euro milioni 100 kwa Atletico Madrid kwa ajili ya Julian Alvarez, huku mchezaji huyo akionyesha nia ya kutafuta changamoto mpya,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Licha ya kocha Diego Simeone kutokuwa chini ya presha ya kumuuza mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kutokana na kuwa na mkataba wa miaka minne iliyobaki, Alvarez ameendelea kuwa mchezaji muhimu baada ya kuhusika kwenye mabao 29 ndani ya mechi 49 alizoichezea Atletico Madrid msimu wa 2025/26.


